Kazi zetu

Kazi kubwa ya TADIO ni kusimamia maslahi ya radio stesheni zinazofika vijijini pamoja na wasikilizaji wake waliopo maeneo hayo kupitia ushawishi wa kuundwa sera bora za kurusha matangazo, mafunzo na kutengeza mtandao kati ya vituo vya radio na kutoa nafasi/fursa kwa washirika wetu kuwafikia zaidi wasikilizaji waliopo vijijini. Muda si mrefu TADIO itaanza radio mtandaoni itakayoitwa Radio TADIO ambayo itatumika kutoa habari mubashara kabisa kwa watu waliopo vijijini.

Kazi ya ushawishi

Kwa niaba ya radio za vijijini zilizopo nchini, TADIO inafanya kazi kubwa kushawishi na kushinikiza serikali pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) juu ya uundwaji wa sera na sheria nzuri zitakozachagiza mazingira mazuri kwa radio za vijijini katika maswala ya urushaji matangazo, tehama, leseni na vibali. Hii ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya radio hizi na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa.

Lengo letu ni kusaidia kutengeneza sera nzuri zitakoruhusu vyombo hivi vya habari kutoa taarifa sahihi kwa wakati sahihi kwa watu waliopo vijijini ambao kwa muda sauti zao zilikuwa hazisikiki.

Kuwajengea uwezo

TADIO pamoja na washirika wetu huwa tunaandaa mafunzo kwa na kuwaalika watangazaji na wazalishaji wa vipindi kutoka radio wanachama wetu. Hii ni kwa lengo la kutengeneza mtandao wa kujuana baina ya radio wanachama wetu nchini Tanzania.

Hivi karibuni radio wanachama wetu walipewa mafunzo juu ya utangazaji wa taarifa kuhusu maswala ya uchaguzi, jinsia, mazingira na maswala ya biashara na kupewa mafunzo ya tehama. Wengine walipewa mafunzo juu uongozi bora na maswala uongozi kwa ujumla. Ifikapo mwaka 2020 tutajikita zaidi kwenye vitendo ili tuweze kuzoea mfumo wetu mpya wa kurusha matangazo kwa njia ya mtandao.

Jinsi ya kuwafikia watu wa vijijini

Idadi kubwa ya watanzania wanaishi vijijini. Kuna asasi nyingi sana zisizo za serikali, taasisi za serikali, mashirika ya misaada na mashirika na biashara ambao wangependa kufikia watu huko vijijini kwa lengo la kuelimisha watu kwenye maswala ya kijamii, afya, kufanya kampeni na pia kutangaza masoko au kutangaza huduma fulani kwa watumaiji waliopo maeneo ya vijijini.

TADIO inaweza kuwa msaada mkubwa kwa maya mashirika/kampuni katika kuwafikiwa watu wa hao wa vijijini kwa kutumia mtandao wa radio zake. Hili linaweza kufanyika kupitia kutengeza ushirika wa pamoja kupitia kudhamini matangazo au vipindi vya radio, hii itaweza kupatia vituo vyetu vya radio kipato kwa ajili ya kujiendesha.

Radio jamii ya mtandao

Radio ya mtandaoni iitwayo Radio TADIO itazinduliwa mwanzoni mwa 2020. Kituo kicho kipya kitakuwa ni kwa ajili ya kutoa taarifa na kufanya matangazo ya radio zinakamata vijijini na kuleta mambo au matukio yanayokea vijijini katika jukwaa la kitiafa.

Radio TADIO itakuwa na kazi ya kuchapisha habari, kupiga picha, habari sauti na kurusha taarifa mubashara kupitia mtandao. Lengo la jukwaa hilo ni kufanya iwe sehemu ambayo inatembelewa na watu wengi ili kujua na kufahamu mada mbalimbali kuhusu watu na mambo ya maeneo ya vijijini. “Kwa uhakika wa habari za vijijini” kama inavyonukuliwa kutoka kwa Mwenyekiti wa TADIO bwana Prosper Kwigize.