Machweo nyuma ya majengo.

BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) WAITEMBELEA  TADIO.

Ujumbe kutoka Baraza la Habari Tanzania walipowasili ofisi za TADIO zilizopo katika Jengo la chuo kikuu Huria Cha Tanzania jijini Dar es salaam.

Bodi ya baraza la habari Tanzania leo tarehe 13/03/2019 wametembelea ofisi za TADIO zilizopo katika jengo la chuo kikuu huria lililopo kinondoni Biafra ambapo pamoja na mambo mengine Baraza wameitaka TADIO kuwashawishi radio wanachama wake kuhakikisha wanashiriki katika Tuzo ili kuongeza chachu ya Utendaji kazi katika vyombo Vyao.

Akitoa neno kwa niaba ya Baraza la Habari Tanzania Edda Sanga ambaye pia alikuwa ni mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) amesema “kuna umuhimu mkubwa sana kwa wana-habari hasa waliopo kwenye vyombo vilivyopo chini ya TADIO kushiriki kwenye Tuzo kwani itawaongezea motisha katika utendaji wao na kuwafanya waipende kazi yao”

Wa kwanza kulia ni Rose Mwalongo -UNESCO ,Marco Shekhalage -UNESCO ,Edda Sanga -MCT Na Saumu Mwalimu toka MCT  Aliyesimama.

 

Aidha Mhariri kutoka baraza la habari Hamis Mzee amesema” Tuzo zinaongeza ufanisi zaidi hasa kwenye kazi yetu ya uandishi hivyo ni muhimu kushiriki kwa kila mwandishi mwenye kigezo cha kushiriki’

Rose Mwalongo kutoka UNESCO anasema”waandishi wamekuwa na uoga wa kushiriki wakidhani kuwa Labda Tuzo ni kwa ajili ya watu flani,nadhani kuna umuhimu sasa wa Baraza la habari kushirikiana na wadau mbalimbali katika wakiwemo UNESCO na wadau wengineo kwa ukaribu zaidi ili kutoa motisha kwa wana-habari kuweza kushiriki zaidi katika siku za usoni”

“UNESCO ndio wamekuwa wafadhili wakubwa wa TADIO chombo hiki ambacho kinaunganisha radio wanachama 31 hivyo nadhani hapa ndio mahala sahihi maana waandishi wengi hasa wamikoani wanatoka kwenye vyombo hivi”amesema Rose

Wajumbe Kutoka Baraza la Habari Tanzania wakipata neno Toka kwa mkuu wa maktaba ya Chuo kikuu Huria cha Tanzania Baada ya kutembelea ofisi za TADIO zilizopo ndani ya chuo hicho.

Awali akitoa changamoto zinazopeleka hasa kwa waandishi wa habari wa radio za kijamii kutoshiriki kwa wingi kwenye Tuzo Afisa mahusiano,Masoko na tehama wa TADIO Bakari khalid amesema”TADIO ina radio wanachama 31 na ina waandishi wengi na wazuri mbao wamekuwa wakizalisha habari na makala nzuri zenye vionjo na kuvutia ,lakini waandishi wa radio hizo hawajawa na muamko wa kushiriki kwenye Tuzo hizo labda kutokana na sababu mbalimbali ,ikiwemo kujiona kama wanyonge kutokana na radio wanazotoka”

“hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Baraza la habari kukuatana na wanahabari ili kujadili kwa kina nini kinapelekea wao kutoshiriki ili kulipatia ufumbuzi wa haraka” amesema Bakari Khalid(hayupo pichani).

Aliyesimama ni Henga Dachi kutoka Idara ya mawasiliano kwa Uma Chuo kikuu Huria cha Tanzania

Ugeni huu uliongozwa na Jaji Mstaafu Juxon Mlay,Eda Sanga, Mellisa Bojang ,Hamis Mzee,, Dinna Chahali na Wallance Maugo na Paul Malimbo.

Ambapo Pamoja na mambo mengine Baraza la habari Tanzania wameahidi kushirikiana na TADIO katika kukuza tasnia ya Habari nchini.