Machweo nyuma ya majengo.

Baraza la Madiwani laipongeza Radio ya Jamii Unyanja.

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa limeipongeza Radio Jamii Unyanja kwa kuwa kiungo muhimu katika uhabarishaji wananchi wa wilaya ya Nyasa.

Pongezi hizo zimetolewa na Alto Komba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa alipokuwa akiahirisha kikao Cha Baraza kilichoketi May 12, mwaka huu.

Alisema Redio Unyanja imefanyakazi ya kutoa habari na elimu juu ya masuala mbalimbali ya Kijamii hali ambayo imechangia kuleta uelewa kwa wananchi.

Baraza hilo pia lilihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stella Manyanya, Viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa Wilaya Isabela Chilumba ,Viongozi wa vyama vya siasa na wakuu wa taasisi za umma.

Credit>> Unyanja FM