Machweo nyuma ya majengo.

Bei ya nafaka yaendelea kushuka mkoani Katavi

Bei ya mazao ya nafaka wilayani Mpanda mkoani Katavi imeendelea kushuka ukilinganisha na miezi mitatu iliyopita.

Baadhi ya wafanyabiashara wameiambia Mpanda Radio kuwa hali hiyo imetokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mikoa iliyokuwa haina chakula kufanikiwa kupata mazao kwa mwaka huu kutokana na mvua zilizonyesha.

Kwa mjibu wa bei ambazo zimetajwa na wafanyabiashara wa masoko ya nafaka Mpanda Hotel na Soko kuu Mpanda Mjini, kwa sasa gunia la mahindi lenye uzito wa kilo 100 huuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 48,000 ikipungua kutoka kati ya Shilingi 48,000 hadi 60,000 huku bei ya mchele ikiwa ni kati ya shilingi 800 hadi 1,100 kwa kilo ikiporomoka kutoka shilingi 12,00 kwa kilo.

Kwa upande wa ulezi bei imepungua kutoka shilingi 750 na kufikia shilingi 675 kwa kilo ambapo gunia lenye uzito wa kilo 100 kwa sasa huuzwa kwa shilingi 67,500 ukilinganisha na shilingi 78,000 bei ya miezi mitatu iliyopita.

Kwa mjibu wa wafanyabiashara,mazao ya nafaka yamekuwa yakisafirishwa kutoka mkoani Katavi kupelekwa maeneo ya Mwanza,Tabora,Dodoma,Shinyanga,Dar es salaam pamoja na nchi jirani kama Congo DRC,Sudani Kusini,Zambia na Msumbiji.

Credit:Mpanda FM