Machweo nyuma ya majengo.

BEST DIALOGUE YAWAFUNDA WASIMAMIZI WA VIPINDI RADIO ZA KIJAMII.

Picha ya pamoja ya washiriki na wakufunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa vipindi wa Radio za kijamii.
Afisa utawala na fedha  kutoka Asasi ya habari za maendeleo ( TADIO )akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Coordinator wa TADIO .
Mwenyekiti wa Asasi ya Habari za maendeleo Tanzania (TADIO) Ambaye pia ni muwezeshaji katika mafunzo hayo akizungumza neno kwa washiriki pamoja na kutoa salam za TADIO.

 

 

 

Moja ya Wakufunzi katika Mafunzo hayo Dotto Bullendu kutoka chuo kikuu cha SAUT Mwanza ,akiendelea na Darasa.
Miriam Mshana Afisa Mawasiliano /BEST DIALOGUE ambao ndio wafadhili wa Mafunzo hayo akizungumza jambo kwa niaba ya BEST DIALOGUE .

 

 

Mkurugenzi wa Dodoma Fm John Baptist (aliyenyoosha kidole) akiwasalimia washirikia pamoja na kuwakaribisha makao makuu ya Nchi.
Pelagia Kijuu Moja ya wakufunzi katika mafunzo haya akiwa makini kufuatilia jambo kwenye kompyuta pakatwa yake.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka kushoto ni Mary Clemence (Mpanda fm),Ospicia Didace Tito (Karagwe fm na Khadija Ali Yusuph (mkoani Fm) wakisiliza darasa kwa makini .

 

Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi wakijadili jambo.
Kutoka kushoto ni Amina Mrisho (Pambazuko Fm) na Gharosi Riwa (Mazingira Fm) wakifuatilia mafunzo kwa umakini mkubwa.
Fredy (Idea Fm) akielezea jambo wakati wa mafunzo .

 

 

                            Washiriki wa mafunzo wakiwa katika kazi za kikundi.
                      Mshiriki  Mary Clemence (Mpanda Fm) akiwasilisha kazi za kikundi.

BEST DIALOGUE kwa Kushirikiana na Asasi ya habari kwa Maendeleo Tanzania (TADIO). yaendesha mafunzo ya siku mbili2 jijini Dodoma, kwa wasimamizi wa vipindi kutoka radio za kijamii 18  ili kukuza Uwelewa kwa wasimamizi hao katika kuandaa maudhui bora kwa jamii..

Mafunzo haya yanakuja wakati ambapo kwa mujibu wa tafiti zinaeleza kuwa vyombo vya habari vya kijamii vimekuwa mstari wa mbele katika kutimiza haja/matakwa ya jamii husika huku vyombo hivyo vikishika nafasi za juu katika kusikiliza na kuzalisha maudhui yaliyo bora kwa jamii .

Awali akifungua mafunzo hayo mwenyekiti wa TADIO Prosper Kwigize ,amewataka washiriki kuwa makini katika kujifunza ili wakawe chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kimaudhui katika vyombo vyao .

Kwigize amesema mafunzo haya kwa ufadhili wa Best Dialogue ni muendelezo wa mipango ya TADIO katika kuwezesha Radio wanachama kufikia malengo waliyojiwekea ya kuwainua vyombo vyao katika maudhuli na ili kujikwamua kuchumi .

Amesema Wasimamizi wa vipindi wana nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko kwenye vyombo vyao,hivyo ni vyema wakazingatia watakayo fundisha ili kujiongezea maarifa Zaidi.

Kwa upande wake Miriam Mshana ambaye ni Afisa Mawasiliano kutoka BEST DIALOGUE,Amesema BEST DIALOGUE inatambua umuhimu wa radio za kijamii ndio maana wameamua kukubali kufadhili mafunzo hayo.

Aidha amesema pamoja na kuwa BEST DIALOGUE inaelekea mwisho wa mradi lakini watatumia fursa waliyonayo kuwaeleza Zaidi wahisani juu ya umuhimu wa kufadhili mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha TADIO kwa wahisani hao ,hivyo kupitia TADIO vyombo vya habari vya kijamii vitanufaika Zaidi.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatatoa tashwila halisi ya utendaji kazi katika vyombo vyetu na kusisitiza kuwa radio ambazo zitaonesha mabadiliko hasa katika uandaaji wa maudhui kama mafunzo yanavyotaka basi radio hiyo itaangaliwa  Zaidi  ili kuweza kunufaika Zaidi na mafunzo mengine baadae.

Awali akiwakaribisha washiriki Afisa fedha na Utawala TADIO Cosmas Lupoja amesema TADIO kama TADIO wataendela kutafuta wahisani Zaidi ili mafunzo haya yawe endelevu na kunufaisha wanachama wote wa TADIO.

miongoni mwa Radio zinazonufaika na Mafunzo hayo ni pamoja na Radio, Dodoma Fm, Fadhila fm, Jamii mtwara, Idea Fm, Pambazuko Fm, Mazingira Fm, Pangani, Jamii fm , Tumbatu Fm, Sengerema Fm.

Nyengine ni Pamoja na Zenj Fm,Kilosa Fm,Kitulo Fm,Uvinza Fm ,Mpanda Fm na Muwakilishi kutoka TADIO.