Fahamu ukweli kuhusu virusi vya corona

TADIO kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Mashirika ya Maendeleo ya kimataifa wamewaandalia mtiririko wa vipindi vya redio kuhusu jinsi ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Kirusi cha corona ni nini? Tunawezaje kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona? Unatakiwa kufanya nini ikiwa umepata maambukizi ya virusi vya corona?

TADIO ikishirikiana na Wizara ya Afya na wahisani wa kimataifa wameandaa mtiririko wa vipindi vinne vikitoa majibu ya maswali mengi kuhusiana na ugonjwa wa corona.

Majibu yote yanatolewa na wataalamu wa afya kutoka Tanzania na Finland. Unaweza kusikiliza vipindi hivyo vya redio vyote hapa chini.




Vipindi maalum kuhusu virusi vya corona vinarushwa na redio jamii 34 Tanzania nzima. Redio jamii hizo hufikia zaidi ya Wasikilizaji milioni 15 Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Vipindi hivi vimetengenezwa na kuletwa kwenu na Mtandao Vyombo vya Habari vya Kijamii (TADIO), Taasisi ya Vyombo vya Habari na Maendeleo ya Ufini (Vikes), Podcast Finland kwa msaada toka Taasisi ya Felm. Ikiwa vimepitiwa, kuidhiniswa na kukubaliwa vitumike kuelimisha jamii na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Tanzania.

Washirika wetu