Fanya kazi nasi

Vipindi vya redio vya kijamii vinasikilizwa sana na jamii za watu wa vijijini na vinakubalika sana. Kuna taarifa nyingi sana za mafanikio kuhusu mabadiliko katika jamii yanayotokana na jitihada zinazofanywa na redio zinazofika vijijini. Tunaweza kuwezesha taasisi au kampuni yako kusikika kupitia redio 43 za kijamii Tanzania, kwa makubaliano binafsi katika eneo moja ama jingine ndani ya nchi.

Fikia wasikilizaji wako

Watanzania walio wengi wanaishi vijijini. Kuna taasisi nyingi zisizo za kiserikali, taasisi za serikali, mashirikia ya misaada na kampuni za biashara zote zenye lengo la kuwafikia watu waliopo vijijini kuwapa elimu kupitia kampeni za afya au kutafuta masoko ya bidhaa na huduma zao kama za simu, kilimo biashara, mbolea, vifaa vya ujenzi, nishati ya jua na usafiri kama pikipiki.

Kupitia TADIO, taasisi yako inaweza kufikia wasikilizaji zaidi ya milioni 33 kupita vituo vyetu 43 vya redio vinavyofika vijijini nchini Tanzania bara na visiwani. Matangazo yanayorushwa na vituo vyetu kwa sasa yanafika zaidi ya 70% nchini Tanzania ambapo maeneo mengi bado hayajafikiwa na vituo vikubwa vya redio.

Kampeni za kutengenezwa kutokana na uhitaji binafsi

Tunaweza kusaidia taasisi au kampuni yako kufikia jamii ya watu waliopo vijijini kupita vituo vyetu vinavyofika vijijini Tanzania Bara na Zanzibar.

  • Kwa kuanzisha miradi shirikishi
  • Udhamini wa vipindi vya redio
  • Kwa kurusha vionjo na matangazo

TADIO inaweza kuanzisha miradi shirikishi ambayo itafanya taasisi yako kuweza kusikika kupitia redio zetu zinazofika vijijini. Matangazo yanaweza kufika eneo moja nchini au mikoa maalumu kwenye maeneo mbalimbali ya kijografia au Tanzania nzima.

Wafanyakazi wetu wenye weledi wanaweza kutengeneza vipindi zilivyodhaminiwa kuhusu kampeni ya mradi wako. Vipindi vitatengenezwa kwa ushirikiano wa hali ya juu vitakahusisha wanajamii katika uandaaji.

Pia kunaweza kuwa na makubaliano maalum na redio mojawapo kati ya wanachama wetu kwa ajili ya kuandaa habari au kudhamini matangazo na vipindi vya majadiliano juu ya mada za elimu, afya, jamii na kampeni mbalimbali kulingana na mada unayokusudia kufanya.

Tunaweza kuzalisha vionjo na matangazo na pia tunaweza kukupa ofa ili uwe uweze kufikia watu wengi zaidi kulingana na eneo unalohitaji.

Redio mtandao

TADIO imekamilisha mchakato wa kuanzisha redio ya mtandaoni ambayo inatoa fursa kwa redio jamii kuchapisha habari na vipindi tofauti kuhusu jamii husika na kuzirusha mtandaoni mubashara. Kupitia ukurasa huo mpya, redio jamii zitakuwa na uwezo wa kuwafikia wasikilizaji nje ya maeneo yao ya kawaida kwakuwa watu wenye simu janja au kompyuta wataweza kutembelea kurasa zetu na kusikiliza moja kwa moja mahala popote mijini na vijijini au hata ukiwa nje ya nchi.

Kupitia matangazo ya mtandaoni kwenye ukarasa wetu mpya au kudhamini matangazo katika vipindi vyetu, unaweza kufikia wasikilizaji wanaosikiliza habari mubashara kabisa kutoka maeneo tofauti vijijini kupita vituo vyetu. Utakuwa na uwezo wa kusikiliza mubashara matangazo yako uliyodhamini kwenye vipindi vyetu ili uweze kufuatilia matokeo ya uwezekaji wako kwenye matangazo. Na zaidi ya hapo, vipindi vya redio vinasambazwa na kusikilizwa kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii. Unaweza kufuatilia zaidi vipindi vyetu mtandaoni uone jinsi gani unaweza kufikia kundi kubwa la watu kote nchini Tanzania.

Unakaribishwa sana kuwasiliana na sisi kwa mazungumzo zaidi kuhusu miradi shirikishi yenye lengo la kuwafikia na kuwahamasisha watu wa vijijini nchini Tanzania.