Machweo nyuma ya majengo.

Kenya wagonjwa wafikia 355.



Miongoni mwa wagonjwa hao, nane wanatokea Nairobi na wanne ni kutoka Mombasa. Watatu kati yao walisafiri kuelekea Somalia hivi karibuni

Katibu Mkuu (Utawala) wa Wizara ya Afya, Rashid Aman pia ametangaza kuwa idadi ya waliopona imefikia 108 baada ya wagonjwa wengine nane kupona

Aidha, Waziri wa Elimu Dkt. George Magoha naye ametangaza kuwa Serikali imeongeza muda wa shule kufungwa kwa mwezi mmoja

Hata hivyo, amefafanua kuwa mitihani ya taifa itaendelea kufanyika, na maamuzi mengine yatategemea uwezo wa serikali katika kudhibiti maambukizi ya Coronavirus

Pia, Kamati ya Dharura ya Kitaifa ya Corona imeagiza zoezi la madereva malori kupimwa katika mipaka yote kuanza mara moja .

#citizen