Young women and young men by a laptop computer

Kuhusu TADIO

TADIO ni mwamvuli wa vyombo vya habari vya kijamii 43 nchini Tanzania (vituo vya redio 43 na Klabu ya Habari ya Pemba). Redio wanachama wetu wote husikilizwa na zaidi ya watu milioni 33 nchini. Tunaamini kuwa “Taarifa ni Nguvu” na usambazaji na upatikanaji wa taarifa ni nyenzo muhimu katika kuchagiza maendeleo ya watu hasa waliopo vijijini na Tanzania kwa ujumla.

Young women and young men by a laptop computer

Tambua

Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), hapo awali ikijulikana kama Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Kijamii Tanzania (COMNETA), ni mtandao wa kutengeneza na kuzalisha habari hasa zenye maudhui ya kijamii nchini Tanzania. TADIO imesajiliwa chini ya Sheria Nambari 24 ya mwaka 2002 ya usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na imepewa cheti namba 0009337.

Kwa sasa kuna redio 43 zinazozalisha vipindi vya kijamii na kurushwa nchi nzima (Tanzania bara na Tanzania visiwani).

Ofisi zetu zinapatikana makao makuu ya Chuo Kikuu Huria Tanzania maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam ambapo pia tuna studio zetu za uzalishaji wa vipindi.

Unakaribishwa sana na pia unaweza kuwasiliana nasi kushirikiana katika miradi mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha jamii ya watu waliopo vijijini na Tanzania kwa ujumla.

Taarifa ni nguvu

TADIO tunaamini kuwa “Taarifa ni Nguvu” hivyo basi hatuna budi kuzalisha na kusambaza taarifa zenye viwango bora hasa kwa watu waliopo vijijini ili waweze kujihusisha moja kwa moja katika shughuli za maendeleo na kujitegemea.

  • Dira yetu: Jamii za vijijini ambazo zinapata na kutumia habari na taarifa za kweli na zenye uhakika kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
  • Dhima yetu: Kuwezesha watu wa vijijini kutumia habari za kweli na uhakika kwa maendeleo yao wenyewe.
  • Kauli mbiu: Fika wasikofika!

Maeneo tunayofikia

Huduma kutoka kwa redio wanachama wetu kwa sasa zinafikia 70% ya eneo la Tanzania na wasikilizaji zaidi ya milioni 33 Tanzania bara na visiwani.

Tuko katika mchakato wa kutengeneza jukwaa la redio za kijamii kwa njia ya mtandao ambao litaruhusu redio za vijijini kuchapisha habari zao na kuruka mubashara katika maeneo yao.

Washirika

TADIO iko tayari kuanzisha ushirikiano wa mahusiano ya kikazi na mashirika ya maendeleo, taasisi za serikali, asasi za kiraia na mashirika ya kibiashara ambayo yana nia ya dhati ya kufikia redio na watu waliopo vijijini kupitia kampeni maalumu zenye udhamnini na matangazo yanayolipiwa.

Kwa sasa tunashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la Maendeleo la Uswizi (SDC) na Taasisi ya Vyombo vya Habari na Maendeleo ya Ufini (Vikes) na wengineo.