Machweo nyuma ya majengo.

LEO NI SIKU YA KIFUA KIKUU (TB) DUNIANI

– Kifua Kikuu (TB) ni miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani na Umoja wa Mataifa (UN) umeripoti kuwa TB inaua watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wowote wa kuambukiza

– Dalili zake ni pamoja na kikohozi cha muda mrefu, kukosa hamu ya kula, kukohoa damu, homa, kutokwa jasho usiku, kupungua uzito na uchovu

– TB ni ugonjwa unaotibika lakini wengi huacha kutumia dawa kabla ya muda waliopangiwa na hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa kuugua kwa muda mrefu zaidi .

-March 24 ya kila mwaka tunaadhimisha siku ya kifua kikuu duniani.