Uzoefu katika Miradi
Kwa miaka iliyopita tumeweza kushiriki katika miradi mbalimbali kama vile elimu, miradi ya afya, miradi ya haki za binadamu na miradi ya maendeleo, inayolenga kuleta athari na mabadiliko makubwa kwa jamii na kuunda uendelevu wa redio za jamii. Haya yamekuwa mafanikio kupitia mafunzo, semina, vipindi vya uhamasishaji na utayarishaji wa jingles, matangazo, vipindi, mijadala, mahojiano na vipindi shirikishi vya redio vilivyoandaliwa chini ya TADIO.