Machweo nyuma ya majengo.

MIUNDOMBINU YA BARABARA NI TATIZO KUBWA JIMBO LA NSIMBO MKOANI KATAVI.

Mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi Mh:Richard Filipo Mbogo .

Mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi Mh:Richard Filipo Mbogo amesema moja ya changamoto inayowakabili wananchi kwa sasa ni miundo mbinu mibovu ya barabara za vijijini.

Mbogo ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara alio ufanya katika Kata ya Kanoge iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi ambapo ameeleza kuwa Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tarura mkoani Katavi inatengewa bajeti ndogo kiasi cha bilioni 3.3 ambazo haziwezi kukidhi mahitaji halisi ya ujenzi na ukarabati wa barabara.

Mbogo ameongeza kusema kuwa kwa kushirikiana na wabunge wenzake kutoka mkoa wa Katavi wanatalajia kutoa mapendekezo ya bajeti ya TARURA iongezeke kutoka bilioni tatu na kufikia angalau bilioni tano.

Katika hatua nyingine amesema upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka kutoka 32% mpaka asilimia 63% kutokana na kuni miradi kadhaa ya maji ikiwemo uchimbaji wa visima vya maji ili kuhudumia wananchi.

#credit
Mpanda Radio FM