Machweo nyuma ya majengo.

MVUA YATENGANISHA VIJIJI -KATAVI

Wasafiri wanaopitia barabara ya Mpanda kwenda Kalema na Ikola Wilayani Tanganyika wamelazimika kuvushwa kwa kubebwa mgongoni baada ya kipande cha barabara katika Kijiji cha Ikaka kutenganishwa na maji ya mto ulio katiza katika barabara hiyo.


Wakizungumza na Mpanda radio fm jioni ya leo wamesema wamekaa katika eneo hilo zaidi ya masaa sita wakisubiri maji ya pungue ili mabasi yavuke jambo ambalo limeshindikana na kulazimu abiria wana fanikiwa kuvuka kwa kubebwa na vibarua walio jiajiri kupakiwa na magari yaliyo Upande wa pili.

Mpanda fm radio imemtafuta Meneja wa Tanroads mkoa wa Katavi ili kujua hatua wanazo chukua kunusuru abilia walio kwama katika eneo bila mafanikio kutokana na kutopatikana kwa simu yake.


Mpanda radiom fm imebaini kuwa eneo hilo halina usimamizi wowote wa usalama wa watu kutokana na shughuri inayofanyika ya kuvusha watu kwa kuwabeba mgongoni jambo ambalo ni hatari maisha lakini uongozi wa wamiliki wa Mabasi mkoani Katavi umelaani kitendo cha serikali kushindwa kuchukua hatua za dharura katika eneo hilo.

Barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa uchumi wa mkoa wa Katavi lakini pia ndio barabara inayo weza kutajwa kimataifa kutokana na kuunganisha pia nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kupitia ziwa Tanganyika.

Credit#MpandaFM