Wanachama wa TADIO
TADIO ina jumla ya wanachama 35 zikiwemo redio jamii 34 na klabu ya waandishi wa Habari Pemba. Redio stesheni hizi 34 zinawafikia Watanzania zaidi ya milioni 33 huku zikiwa na wasikilizaji Tanzania bara na visiwani ikiwa ni takribani asilimia 70 ya eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. TADIO ipo katika mchakato kutengeneza jukwaa la redio jamii mtandaoni ambapo redio hizi zitaweza kurusha matangazo mubashara na vipindi mbalimbali.
Ifuatayo ni orodha redio jamii ambazo ni wanachama hai wa TADIO.