Machweo nyuma ya majengo.

Rais John Pombe Magufuli Aongoza Watanzania Katika Mazishi Ya Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Tatu Benjamin William Mkapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa, Mama Anna Mkapa wakati wakielekea kuweka Udongo kwenye Kaburi la Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Kijijini Lupaso Masasi mkoani Mtwara
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo akitoa heshima baada ya kuweka udongo katika kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, na kisha akapiga saluti kama ishara ya heshima.
Wanajeshi wakitoa heshima zao za mwisho kwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa katika mazishi yako Lupaso, Masasi mkoani Mtwara.