Machweo nyuma ya majengo.

RAIS MUSEVENI AWAONYA WENYE NYUMBA, ATAKA WAPANGAJI WASIFUKUZWE

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa onyo kwa wapangaji nchini humo na kuwataka wasiwafukuze wapangaji wanaoshindwa kulipa kodi katika wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliana na janga la Corona

Museveni amesema huu sio mwisho wa dunia na kwamba wenye nyumba wanapaswa kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga hili litakapoisha, madeni yote yatalipwa

Pamoja na hayo, Rais Museveni pia amewaagiza Polisi nchini humo kuingilia kati pale wanapokuta mpangaji anafukuzwa .

credit#jamiiforum