Redio wanachama wa TADIO kunufaika na msaada wa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kutoka UNESCO

Jana, UNESCO ilitoa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa Wanahabari chini ya Shirika la Habari la Maendeleo la Tanzania, mwavuli wa Redio ya Jamii ya Tanzania. Msaada huu wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 unakusudia kuiwezesha TADIO na wanachama wake kujilinda na magonjwa ya milipuko katika shughuli zao za kila siku. Msaada huo uliwasilishwa na Bwana Tirso Dos Santos mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania na Mwenyekiti wa TADIO, Bwana Prosper Kwigize kwa niaba ya TADIO na wanachama wake.

Wakati wa makabidhiano, Bwana Tirso alisema kuwa UNESCO imeguswa na mazingira salama kwa Wanahabari na wanatumai kuwa vifaa hivyo vitawawezesha kufanya kazi kwa usalama katika mazingira hatarishi au magonjwa ya milipuko kama Ebola, mafua, COVID19 na Chlorella.

Mwenyekiti wa TADIO Bwana Kwigize alishukuru ushirikiano kati ya UNESCO na TADIO na kwa msaada uliotolewa kwa mtandao wa Redio ya jamii nchini Tanzania. Vifaa vitasambazwa kwa watendaji wa redio zaidi ya 300 nchini kote.