Machweo nyuma ya majengo.

SERIKALI YAKANUSHA UWEPO WA UHABA WA SUKARI NCHINI

Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuna akiba ya kutosha ya sukari huku zaidi ya tani 10,000 za ziada zikiwa zimewasili bandari ya Dar es Salaam na kuanza kusambazwa kwenye masoko na kukanusha bidhaa hiyo muhimu kuadimika nchini.
Waziri Bashungwa amelazimika kutoa ufafanuzi huo jijini Dodoma baada ya kuwepo kwa taarifa ya kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo mara dufu huku kwenye baadhi ya masoko ya jiji hilo sukari ikiuzwa kati ya shilingi 4000 mpaka 4500 kutoka shilingi 2400.

“Serikali imeunda timu ya kuchunguza kubaini kama kuna wafanyabiashara wamehodhi ili kujipatia faida na sheria itachukua mkondo wake,” amesema Waziri Bashungwa.
Bashungwa anasema hivi sasa asilimia 80 ya sukari inazalishwa nchini huku iliyobaki ikiagizwa nje na hivi karibuni serikali ilitoa kibali cha kuagizwa kwa tani 10000 kutoka nje na tayari zimeshawasili.