Serikali
imetaja sababu tatu ambazo zimesababisha kuadimika kwa sukari nchini,
huku ikitoa msimamo wake kuhusu bihaa hiyo muhimu.
Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema bungeni jana kuwa sababu hizo ni
ugonjwa wa corona, baadhi ya wanunuzi kuficha sukari, meli nyingi
zimekuwa zikifaulisha mizigo kwenye meli nyingine hivyo kusababisha
kuchelewa kufika kwa wakati nchini.
Hasunga
alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake
ya mwaka wa fedha 2020/21 jijini Dodoma, ambapo aliomba Bunge
liwaidhibishie zaidi ya Sh bilioni 229.8.
Kutokana
na hali hiyo, alisema kuwa ili kukabiliana na na changamoto ya ukosefu
wa sukari, Serikali ilitoa vibali vya kuagiza sukari tani 40,000 kutoka
nje ya nchi.
Alisema
kikao cha pamoja na wawakilishi wa uzalishaji, Serikali na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Bodi ya Sukari chini ya usimamizi wa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, walikubaliana kutokupandishwa kwa bei za
sukari.
“Hata
hivyo kumejitokeza kuchelewa kuingia nchini kutokana na Covid-19 ,
baadhi ya wanunuzi kuficha sukari imekuwa ni tatizo. Wizara kupitia Bodi
ya Sukari ilifanya uchunguzi wa kina na kwa kutumia sheria ya tasnia ya
sukari ilichukua hatua ya kutangaza bei elekezi ya jumla na rejareja
katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa lengo la kukabiliana na
wafanyabiashara wasio waaminifu.
“Sasa
hivi ni kweli katika maeneo mbalimbali kuna upungufu wa Sukari, ni
kutokana na meli nyingi zimekuwa zikifaulisha kwenye meli nyingine hivyo
haiji kadri unavyotakiwa,” alisema Hasunga.
Hasunga
alisema mpaka kufikia Mei 10 mwaka huu tani zilizokuwa zimewasili
nchini ni 4,000 huku tani 21,000 zikitarajiwa kuwasili mwezi huu.
“Tani
500 zimetoka Afrika ya Kusini zimeshafika hivyo hatutegemei kuwa na
upungufu wa sukari, mahitaji ni tani 35,000 kwa mwezi hivyo
ilivyoingizwa ni tani 40,000 na waliamini itatosha maana viwanda ilikuwa
vianze uzalishaji Mei mwishoni.
“Lakini
kutokana na mvua kuendelea kunyesha na kiwanda kimoja tu kimeonyesha
dalili ya kuanza uzalishaji mwisho wa mwezi,” alisema Hasunga.
Aidha Waziri huyo wa Kilimo, aliwatoa hofu Watanzania kwa kudai kwamba Sukari ipo ya kutosha.
“Niwahakikishie
Watanzania kuwa Sukari iliyoingia na hatua zilizochukuliwa kwani sukari
inatosha kabisa na hatuhitaji kuwa na upungufu. Niwaombe wenzangu
wanaohusika wahakikishe sukari iliyofika wanaiotoa na kusimamia
usambazaji katika mikoa yote nchini.
“Tumekokotoa
bei ya sukari inayotoka nje mpaka inafika Dar es Dalaam ni Dola 350
(zaidi ya Sh 800,000), mpaka nchi za mbali kama Brazil ni dola 500
(zaidi ya Sh milioni moja) , tukikikokotoa kwa bei ya Tanzania Sukari
haitakiwi kuzidi bei tulizotangaza,” alisema.
Waziri
Hasunga alisema walikaa kikao na Waziri Mkuu na waagizaji wa Sukari
nchini ambapo wagizaji hao walikubali kutopandisha bei ya sukari.
“Na
tumekaa jana (juzi) chini ya Waziri Mkuu na waagizaji wa Sukari
wametuahidi kabisa bei haitakiwi kupanda hivyo katika sukari inayokuja
itauzwa kwa bei ile tuliyoizoea,” alisema.