Machweo nyuma ya majengo.

SHULE YA SEKONDARI MWERA KUPOKEA WANAFUNZI 80 WA KIDATO CHA TANO

Shule ya sekondari MWERA iliyopo kata ya MWERA wilayani Pangani mkoani TANGA inatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha tano julai 20 mwaka 2020.

Akitoa taarifa hiyo katibu tawala wia Wilaya ya Pangani mwalimu HASSANI NYANGE ametaja idadi ya wanafunzi watakaofika kwa awamu ya kwanza kuwa ni 80 na wote ni wasichana huku maandalizi ya Walimu, na zana za kufundishia tayari zimeshawasilishwa shuleni hapo.

Mwalimu NYANGE ameelezea baadhi ya changamoto zilizotatuliwa katika shule hiyo ikiwemo umeme, jiko, vitanda, na uwepo wa miundombinu ya maji ili kukamilisha huduma shuleni hapo.

Pia amewataka wakazi wa Wilaya ya Pangani na Wilaya za jirani kuitumia Shule hiyo kama fursa ya maendeleo kwa kuwa Shule hiyo inapokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali.

Aidha amewasisitiza wananchi wanaoishi karibu na Shule hiyo kuitumia fursa kwa kujishughulisha na biashara mbali mbali ili kujipatia kipato.

Shule ya kidato cha Tano na Sita Mwera ni ya michepuo ya sanaa kwa wasichana inafanya idadi ya shule hizo kuwa mbili wilayani Pangani ambapo awali ilianza shule ya Tongani ambayo kwa mwaka huu wa 2020 inachukuwa wanafunzi kwa awamu ya tatu michepuo ya sayansi.

#panganiFM