Machweo nyuma ya majengo.

TADIO WAISHUKURU UNESCO KWA KUENDELEA KUWASHIKA MKONO.

 

Mwenyekti wa Asasi za habari kwa Maendeleo Tanzania Prosper Kwigize akizungumza na wajumbe kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa TADIO.

 

Wajumbe wa mkutano mkuu wa TADIO wakiwa wanafuatilia jambo kwa makini.
Ayubu Kalufya Mkurugenzi wa Uvinza FM (KIGOMA) na mjumbe wa mkutano mkuu ,akichangia jambo kwenye mkutano kwenye mkutano mkuu wa TADIO ,unaofanyika Dodoma.

 

Frederick Meela Mkurugenzi Radio Kwizera na mjumbe wa mkutano mkuu wa TADIO akisalimia wajumbe wengine.
Cosmass Lupoja Afisa utawala na fedha TADIO akiwasilisha mpango kazi wa mwaka ,kwenye mkutano mkuu wa TADIO unaofanyika Leo jijini Dodoma .
Maria Lembeli mkurugenzi wa Kahama FM Radio (KAHAMA) na mjumbe wa mkutano mkuu akifuatilia taarifa za ukaguzi wa fedha za TADIO kwenye mkutano mkuu wa mwaka.

 

Irene Makene Mratibu wa Asasi ya habari za Maendeleo Tanzania TADIO akisalimiana na wajumbe wa mkutano mkuu wa Mwaka unaofanyika Dodoma kwenye Ukumbi wa Nala Hotel.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa TADIO katika picha ya pamoja.

Taasisi ya habari za maendeleo Tanzania (TADIO) wameishukuru UNESCO kwa kuendelea kuwashika mkono katika kuzisaidia Radio za kijamii nchini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma  na  Mwenyekiti wa TADIO Prosper Kwigize kwenye mkutano mkuu wa Mwaka ambao unafanyika kwenye ukumbu wa Nala Hotel Jijini humo.

Kwigize amesema UNESCO wamekuwa na mchango mkubwa katika kuikuza TADIO ikiwa ni pamoja na Radio wanachame wake.

“Tumekuwa na vikao vya mara kwa mara na UNESCO kuona namna gani ya kuendelea kuzisaidia Radio wanachama wa TADIO ,hii ni katika kuhakikisha wanahabari wanajengewa uwezo wa kitaaluma lakini pia Vyombo vyetu viweze kutoa maudhui yaliyo bora zaidi”

“Kwa mujibu wa tafiti za mwaka huu zinaonesha Radio za kijamii ndio zimeongoza katika maudhui bora na yenye kukidhi mahitaji ya Jamii.”amesema Kwigize .

Jumla ya wajumbe 32 wa mkutano mkuu wako Dodoma katika mkutano huo.

UNESCO wako Jijini Dodoma  katika Mafunzo ya siku 5 ya wanahabari kutoka Radio wanachama wa TADIO ,ambao wanajengewa uwezo juu ya Afya ya uzazi,Ukimwi,Ukatili wa kijinsia na Elimu kwa Wasichana .