Kaimu Meneja wa Uyui FM, Bi. Nyamiz Mdaki akikabidhiwa vifaa vya kujikikinga na magonjwa ya mlipuko na Mwenyekiti wa TADIO, Bw. Prosper Kwigize

TADIO yaanza kusambaza vifaa vya afya kutoka UNESCO

Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) limeanza kusambaza vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko vilivyotolewa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa vituo vya redio jamii chini ya mwamvuli wa TADIO.Vifaa hivi vyenye thamani zaidi ya TZS milioni 10 vinakusudiwa kufikia zaidi ya watendaji 300 wa redio na kusaidia waandishi wa habari kutoka vituo hivyo kujikinga na magonjwa ya milipuko katika shughuli zao za kila siku.

Meneja wa Dodoma FM, Bi. Zania Miraji akikabidhiwa vifaa vya kujikinga ma magonjwa ya mlipuko na Mwenyekiti wa TADIO, Bw. Prosper Kwigize


Wakati wa makabidhiano, mwenyekiti wa TADIO, Bwana Prosper Kwigize aliwataka mameneja wa redio wanachama wa TADIO kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatumika vizuri na vinamfikia mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwandishi wa habari haswa waandishi wa habari wanawake.

Meneja wa Sibuka FM, Bw. Daniel Manyanga akikabidhiwa vifaa vya kujikikinga na magonjwa ya mlipuko na Mwenyekiti wa TADIO, Bw. Prosper Kwigize
Meneja wa Sibuka FM, Bw. Daniel Manyanga akikabidhiwa vifaa vya kujikikinga na magonjwa ya mlipuko na Mwenyekiti wa TADIO, Bw. Prosper Kwigize


Mameneja wa redio wanachama wa TADIO waliishukuru UNESCO na TADIO kwa msaada unaojali usalama wa wanahabari wa redio zao na waliahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa.

Tazama picha zaidi hapo chini: