Machweo nyuma ya majengo.

TMA Yatoa tahadhari ya mvua kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imewataka Wakazi wa Dar, Tanga, Pwani, Mafia, Unguja na Pemba kuchukua tahadhari kutokana na maeneo hayo kutarajiwa kupata Mvua kubwa kuanzia leo Oktoba 29, 2023 TMA imeonya kuwa Mvua zitanyesha kwa siku 3 na zinaweza kubabisha Mafuriko pamoja na kuharibu shughuli za Kiuchumi hivyo Wananchi waepuke misongamano wa Watu, pia, wahifadhi mahitaji muhimu ndani Awali, TMA ilitabiri kuwa Tanzania inatarajia kukumbwa na Mvua za El Nino kuanzia Oktoba ambapo tayari Mikoa ya Tanga, Pemba na Unguja imeripotiwa kupata Mvua zinazozidi Milimita 50.