









Na Bakari Khalid
Dodoma
Waandishi wa habari 18 kutoka radio za kijamii leo wametembelea Idara ya habari maelezo ,kujifunza na kufahamu kwa undani shughuli za Idara hiyo .
Akizungumza kwa niaba ya wengine Mwenyekiti wa Asasi ya habari kwa maendeleo Tanzania (TADIO) Prosper Kwigize amesema wameishukuru sana idara ya habari maelezo kwa kukubali mualiko wao ,kwani ni fursa hadhimu ambayo pamoja na mambo mengine wamepata kujadili maswala mbalimbali yanayohusu taaluma ya habari.
Kwigize amesema vyombo vya habari vya kijamii vina mchango mkubwa ,hivyo ni vyema vikapewa kipaumbele kwa ndio vyombo pekee vilivyo karibu na jamii .
Akitoa malalamiko juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika sehemu zao za kazi moja ya waandishi hao Amina Mrisho (Pambazuko FM) amesema kumekuwa na changamoto sana kwa waandishi vyombo vya kijamii kwa wanakosa ushirikiano kwa maafisa habari wa wa mikoa.
“Wamekuwa wagumu sana kutoa ushirikiano hasa wakijua kuwa ni mwandishi habari kutoka vyombo vya kijamii” Amesema Amina .
Kwa upande wake Rodney Mbuya Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari maelezo makao makuu Dodoma,amesema amefurahishwa na ujio wa wana habari,kwani tasnia ya habari ina mchango mkubwa sana katika kufikisha taarifa kwa wananchi.
Aidha amewataka waandishi kuwatolea taarifa kwa viongozi wao wale maafisa habari wanaokataa kutoa ushirikiano kwao,hivyo wao kama Idara kupitia wizara ya habari Sanaa utamaduni na michezo watafanyia kazi swala hilo ili wananchi waweze kupata taarifa za uhakika na kwa wakati kupitia vyombo hivyo vya kijamii kwani ndio hasa viko karibu na wananchi.
Mbuya amewataka waandishi kufanya kazi yao kwa ajili ya kizazi kijacho huku akitolea mfano taifa la china lilivyofanikiwa kwa kufanya hivyo mpaka sasa wanavuna matunda ya wazee wao.
Aidha Mbuya amewataka kuchangamkia fursa ya kupata press card ili kutambulika na Idara hiyo lakini pia itasaidia kupunguza watu wanaoichafua tasnia hiyo (kanjanja).
Jumla ya waandishi wa habari 18 kutoka radio za kijamii wapo mkoani Dodoma kwenye mafunzo ya kuwaongezea uwezo katika kuzalisha maudhui bora,Mafunzo haya yameandaliwa na TADIO kwa ufadhili wa BEST DIALOGUE.