Picha ya pamoja.



Waandishi wa habari wa radio jamii nchini wametakiwa kuweka mazingira ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuipa kipaumbele katika usambazaji wa taarifa hasa kwa watu wa maeneo ya vijijini.
Hayo yamejiri wiki hii jijini ARUSHA katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa radio jamii 25 kutoka Tanzania bara na Zanzibar ambayo yalikuwa na lengo la kuwawezesha waandishi hao kutumia vyema Tehama na takwimu katika habari wanazozizalisha katika vituo vyao.
Wakizungumza mwishoni mwa mafunzo waandishi hao wamesema awali walikuwa hawatambui ni kwa namna gani watapeleka taarifa na vipi watapata mrejesho wa taarifa hizo kutoka wa wasikilizaji hivyo kupitia mafunzo hayo wametambua namna njema ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
‘’suala la ICT,ni matumizi ya Tehama katika habari, na hata katika vituo vyetu vya radio tulikuwa hatutambua ni namna gani tunapeleka habari vijijini, lakini pia namna gani tunapokea feedback kutoka kwa wasikilizaji wa vijijini mwanzoni tulikuwa tunafanya tuu lakini tulikuwa hatufahamu kama kuna kurudisha mrejesho kwa kutumia Tehama. Na kwa upande wa taarifa zetu ni kwamba passward inaulazimu wa kubadilisha mwanzo ilikuwa tunatumia na tunakaa miaka miwili hujabadilisha passward kwa hiyo tumejifunza namna ya kuweka passward ambayo itamsababisha mtu ashindwe ku attack taarifa zako.’’ Amezungumza mmoja wa wanahabari.
‘’yule ambaye ameamua kuuza computer yake ambayo ameitumia hatujui amekumbana na nini hadi akaamua kuiuza katika mafunzo haya nimejifunza ni bora ununue kifaa ambacho hakijatumia ili ajuwe kimeingiliwa au hakijaingiliwa na virus na upande wa kutumia taarifa katika mitandao ya jamamii tulikuwa tunaona ni jambo dogo kumbe ni jambo kubwa ambalo litatunufaisha.’’ Ameongeza kusema mwanahabari mwingine.
Kwa upande wa muwezeshaji kutoka shirika la umoja wa mataifa elimu, sayansi na utamaduni bwana LEONARD KISEMA amewashukuru wanahabari hao kwa mrejesho walioutoa baada ya mafunzo huku kusisitiza uendelevu wa suala la usalama wa vifaa wanavyotumia.
‘’nashukuru kwa feedback ambazo nimezisikia kutoka kwa kila mmoja wenu,ingawa kidogo zimenistua, kitu ambacho nimestuka ni kwamba kumbe tatizo la usalama katika vituo vyenu vya radio, usalama wa IT ni kubwa kuliko nilivyokuwa nafikiria mwanzo, nimesikia watu wengi wamekuwa na shida computer zao, wametupa computer,wameharibu data,wamepata hasara nyingi nafikiri tukikaa sasa hapa tukafanya utafiti, mdogo hasara ambazo vituo wamepata kwa sababu ya malware, kwa sababu ya virus, unaweza ukashangaa, kwa hiyo suala la usalama wa vifaa ni suala endelevu na suala ambalo tunapaswa kuliishi katika maisha yetu binafsi.amesema bwana LEONARD KISEMA
Bwana AJUAE MDEGELA ni mkufunzi kutoka chuo kikuu cha tumaini pia muwezeshaji katika mafunzo hayo amewataka wanahabari wa radio jamii kutumia mafunzo hayo na kuambukiza wengine katika vituo vyao.
‘’kuhusiana na mafunzo mimi naomba mkitoka hapa mkayatendee haki, haya mafunzo mliyoyapata, nataka feedback nijuwe kabisa uyu ameandika habari na ametumia vyanzo vya mitandao website au mitandao ya kijamii, yaani hii uliyoipata wewe ilikuwa ni share ya kituo chako chote, kwa hiyo ukitoka hapa hakikisha yale yote mliyojifunza hakikisha mnafanya kazi kwa lengo hili moja. Amemalizia bwana AJUAE MDEGELA
Mafunzo hayo ya matumizi ya mitandao kwa wanahabari yamekwenda sambamba na usalama wa matumizi ya vifaa kama vile computer na simu hivyo wamewezeshwa njia mbali mbali za kuvilinda vifaa vyao na wametakiwa kuweka sera zitakazotumika ili kujiepusha na hasara zitokanazo na virus wanaoshambulia taarifa.