Machweo nyuma ya majengo.

Wanahabari watakiwa kuandika zaidi habari za wanawake na watoto

Libe Mathias Chonya -Moja ya wakufunzi akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo .
Mafunzo yakiendelea
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia jambo kwa makini.
Kutoka kushoto ni Saumu Bakari (Mratibu wa Mradi-TADIO)akijadiliana jambo na Moja wa wakufunzi wa mafunzo haya Bw: Bujo Ambosisye .

Waandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuibua na kupaza sauti za wanawake ,watoto vijana katika nyanja mbalimbali.

Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa chuo Kikuu Huria (OUT), Libe Mathias  Chonya wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari juu ya namna ya kuripoti taarifa za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wananawake na watoto.

Chonya ameongeza kuwa  endapo kama jamii itakuwa na uelewa juu ya madhara yatokanayo na ukatili ya kijinsia kwa wanawake na watoto itasaidia kuleta  usawa wa kijinsia pasipo ukatili.

Kwa upande wa wandishi wamepokea vyema mafunzo hayo na kusema kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu ya kuleta mabadiliko kwa jamii has katika kuandika  habari za kijinsia na watoto.

“Kwa Tunawashukuru TADIO na wadau wote waliohusika katika kuandaa mafuzo haya ,kwani yatatujengea uwezo sisi kama waandishi hasa katika kupinda maswala ya ukatili wa aina zote kwa jamii” Amesema Amua Rushita –Mwandhishi wa habari kutoka Jamii FM mtwara

Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari (YOUNG REPORTERS  yanasimimiwa na Asasi ya vyombo vya kijamii Nchini TADIO kwa ushirikiano wa WE World,KIWOHEDE,TBI, DLAB kufadhiliwa na European Union(EU) lengo la mafunzo haya kuwawezesha waandishi wa habari  kuibua na kuandika habari za kijamii zinazohusu ukatili wa kijinsi,vijana na kufahamu sheria pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

Mafunzo haya ya siku 10 yameanza August 31  yanafanyika katika ukumbi wa  mikutano wa TCCIA mkoani Mtwara .