Machweo nyuma ya majengo.

Waziri Jafo aagiza kuchunguzwa kwa Halmashauri ya Mlele Mkoani Katavi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Seleman Jaffo ametoa agizo kwa Katibu mkuu wa TAMISEMI kuunda tume ya kuchunguza Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoani katavi kutokana na kusuasua kwa mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.
Maagizo hayo ameyatoa jana katika ziara yake mkoani Katavi ambapo amesema kuwa halmashauri hiyo imekuwa na mambo ya hovyo ambayo yamekuwa yakichafua mkoa wa Katavi akitolea mfano udanganyifu wa tofali zaidi Elfu sabini na tano zilizobainika kuwa feki pamoja ikiwemo kutokulipwa kwa wafanya biashara ambao wanadai Halmashauri hiyo kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine amewapongeza watumishi na mkuu wa mkoa wa katavi Juma Zuberi homera kwa kusimamia vizuri pesa zinazotelewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama ujenzi wa vituo vya afya mkoani Katavi
Sanjari na hayo Jafo ameagiza afisa manunuzi wa wilaya hiyo arudishwe maramoja katika wilaya hiyo licha ya kuwa amehamishiwa eneo lingine baada ya kukutwa na tuhuma.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera amesema vituo vya Afya 7 vimejengwa na vimeanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa Hospital 3 ambazo Kila wilaya inatakiwa ijenge hospila moaja.

Baada ya kupokea taarifa hiyo ambayo imetolewa katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Waziri Jaffo amefanya ufunguzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 7.7 iliyopo katika Manispaa hiyo ambayo ni mradi wa serikali kwa kushirikiana na Benki ya dunia.

Na: Mpanda FM