Machweo nyuma ya majengo.

WAZIRI MKUU AELEZEA HALI YA MAAMBUKIZI YA CORONA MPAKA SASA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema, hadi Aprili 21, 2020 jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na #COVID19; Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, 7 wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki

Mara ya mwisho Waziri wa Afya alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa COVID19 ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka

Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)

Waziri Mkuu ameyasema hayo akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa huu yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar

Pia, amsema Rais Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu wamemtuma awasilishe salamu za uepndo na shukrani kwa wote wanaoonesha jitihada katika kupigania maisha ya watu wote hapa nchini .

credi #Jf