Machweo nyuma ya majengo.

ZANZIBAR YATANGAZA WAGONJWA WAPYA 7 WA COVID19

Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa 7 wa COVID19 idadi inayofanya kuwa na jumla ya visa 105.

Jumla ya wagonjwa 36 wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani, wakishauriwa kubaki ndani kwa siku 14 huku wataalamu wa Afya wakiendelea kuwafuatilia.

Serikali imetoa wito kwa wananchi kuendeea kuchukua tahadhari. Pia kwa wenye dalili wametakiwa kupiga simu namba 190.

Wizara ya Afya imevitaka vyombo vya habari kupata taarifa za CoronaVirus kutoka Wizara ya Afya.